Ijumaa , 21st Mar , 2014

Msanii Diamond Platinumz, amesema kuwa, kwa sasa baada ya mafanikio makuwa ya remix ya ngoma yake ya My Number One, picha linaendelea ambapo atawazawadia mashabiki wake kolabo nyingine kubwa ya kimataifa hivi karibuni.

Diamond amesema kuwa, harakati anazofanya sasa ni kufanya Tanzania na muziki wake ufike mbali zaidi, ambapo amefichua kuwa, amekuwa akipokea maombi mengi kutoka kwa wasanii wa nje kwa ajili ya kufanya kolabo nae, na hapa anaeleza juu ya mchongo huu, vile vile kolabo nyingine za kimataifa ambazo zitatoka baada ya My Number one Remix.

Msanii huyu amesema pia, baada ya kuusoma vizuri muziki barani Afrika, amegundua kuwa kuna soko kubwa la muziki wa Afrika Magharibi, na pia kuna soko la muziki wa Afrika kwa ujumla, na sasa atakua akitoa ngoma zake kwa kufuata ramani ya soko hili.

Diamond pia amewakata mashabiki wake kufahamu kuwa, hivi karibuni kuna kazi kubwa ambazo amefanya na Iyanya pamoja na D'banj ambao ni wasanii wakuba Nigeria, kazi ambazo zinatarajia kutikisa vilivyo pindi zitakapotoka.