Jumamosi , 1st Mar , 2014

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Desire Luzinda anatarajiwa kurudi jukwaani kwa kishindo akiwa na nguvu mpya baada ya miaka 6 ya utulivu, ambapo amepanga kutumbuiza katika onyesho la aina yake ambalo amelipatia jina 'Black and White Affair'.

Onyesho hili litafanyika tarehe 6 mwezi June na linatarajiwa kuvuta wapenzi wengi hasa kutokana na mwanadada huyu kukaa kipindi kirefu bila kufanya onyesho aliloliandaa mwenyewe.

Kwa sasa pia msanii huyu anaandaa video ya kazi yake inayokwenda kwa jina Equation ambayo anatarajia kuifanya na watararishaji video mahiri wa Ogopa DJ's kutoka Kenya.