
Msanii Dayna Nyange
Akiwa jijini Lagos nchini Nigeria kwa shughuli zake mbalimbali ikiwa ni pamoja na muziki, Dayna amethibitisha kukamilika kwa projects zake kibao ikiwa ni pamoja na EP yake ambayo itakuwa ya kwanza kupitia mahojiano ‘’Moments With Dayna Nyange’’ huku kukiwa na collabo za ndani na kimataifa za kutosha.
Star huyo aliyewahi kutikisa kupitia kazi zake kama ‘Komela, Mafungu ya nyanya’ muda wowote ataweka wazi cover ya EP na tracklist.