Alhamisi , 28th Aug , 2014

Dabo, Msanii ambaye anafanya poa katika miondoko ya Ragga na Dancehall hapa Tanzania, baada ya kufanya vizuri na project ya Mimi na Wewe, ametangaza kutoa zawadi kwa mashabiki wake hapo kesho kupitia EATV.

msanii wa muziki wa reggae na dancehall nchini Dabo

Dabo amesema kuwa, tayari amekwishakamilisha ujio wake mpya, audio na video ya mahadhi ya Sweet Reggae inayokwenda kwa jina I Love You.

Dabo aliyechaguliwa kuwania tuzo za kimataifa nchini Marekani ametoa shukrani kwa sapoti ambayo tayari ameanza kupata.