Alhamisi , 8th Jan , 2015

Msanii nyota nchini Nigeria Oladapo Daniel Oyebanjo aka D’Banj imeelezwa kuwa ameingia katika uhusiano wa mapenzi na mrembo kutoka nchini Afrika Kusini anayejulikana kwa jina la Bonang Matheba.

Msanii wa muziki wa nchini Nigeria D'Banj akiwa na mpenzi wake Queen B

D'Banj ambaye awali alizama katika dimbwi la mapenzi na wanawake mastaa wa kinigeria akiwemo muigizaji nyota Genevieve Nnaji na mtoto wa tajiri Adama Ndimi, tayari ameonesha kuzama kwa mrembo huyo wa nchini Afrika Kusini.

Imeelezwa kuwa mpenzi wake huyo Bonang Matheba almaarufu kama Queen B ni mtangazaji wa Luninga na Radio, mwanamitindo na balozi wa bidhaa maarufu za urembo nchini humo.