Country Boy uso kwa uso na Davido

Jumamosi , 1st Mei , 2021

Ni 'Headlines' kutoka nchini Nigeria ambapo kwa mara ya kwanza msanii HipHop Bongo Countyr Boy amekutana na staa wa Taifa hilo na Africa kwa ujumla bwana Davido Adeleke 'OBO'.

Picha ya Country Boy na Davido

Country Boy ameshea picha hiyo akiwa na Davido kwenye ukurasa wake wa Instagram huku ameandika kuwa "Kabla ya maswali ya collabo kwanza mnaweza kutumia hii picha kwa matumizi mengine".

Country Boy na Ibraah ni baadhi ya wasanii kutoka lebo ya Konde Music Worldwide kwa sasa wapo nchini Nigeria katika maandalizi ya Album ya CEO wao mtu mzima Harmonize.