Alhamisi , 3rd Sep , 2015

Msanii wa muziki wa nchini Uganda, Cindy Sanyu ameripotiwa kuwa mafichoni akisakwa na polisi baada ya tukio la kumshambulia hasimu wake, msanii wa muziki Phina Mugerwa ambaye kwa muda sasa wamekuwa hawaelewani.

Ken, Cindy & Phina

Sababu kubwa ya kutokuelewana kwa pande hizo mbili ni kutokana na Cindy kutoka kimapenzi na baba wa mtoto wa Phina.

Cindy ametajwa kufanya tukio hilo kwa kumfuata Phina katika baa moja maarufu huko Kampala na kumsababishia fujo, akimuonya kukaa mbali na Ken ambaye ni mpenzi wake, kitendo ambacho kilipelekea Phina kufungua mashtaka polisi.

Mpaka sasa Cindy hajaweza kuonekana wala kulitolea ufafanuzi tukio hilo, huku ikielezwa kuwa bado anahitajika kituoni kwaajili ya kutoa maelezo yake ya utetezi.