Jumapili , 7th Jun , 2015

Nyota wa muziki wa miondoko ya injili Christina Shusho ametoa wito kwa wasanii na pia vijana ambao hivi sasa wanajiandaa kwa ajili ya uchaguzi mkuu uanaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 25 nchini Tanzania.

Mwimbaji wa miondoko ya muziki wa injili Christina Shusho

Christina ambaye hivi sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya 'Ninang'ara ameongea na enewz kuhusina na uchaguzi huo mkubwa akiwalenga zaidi vijana kutambua kuwa ni jukumu lao kubwa kumchagua kiongozi ambaye ataleta mabadiliko katika nchi.