Jumapili , 2nd Jun , 2024

Staa wa muziki Chris Brown amekataa kufananishwa na marehemu Michael Jackson baada ya wasanii wakubwa na mashabiki kutaja jina lake kama ndiyo mrithi wa aliyekuwa mfalme huyo wa Pop Duniani.

Picha ya Chris Brown na Michael Jackson

Chris Brown anasema yeye sio bora kuliko Michael Jackson na hakuna wa kushindana naye kwa sababu angekuwepo hai asingeweza kupumua wala kuimba mbele yake.

“Mtazamo wangu wa binafsi ni kwamba nisingeweza kupumua au hata kuimba wimbo ikiwa mtu huyo angekuwapo. Hakuna kushindana naye, mimi si bora kuliko Michael Jackson”. amesema Chris Brown

Rapa na muigizaji 50Cent ni moja ya wasanii wanaoamini ChrisBrown ni mrithi wa MJ.

Pia Fat Joe anasema Chris Brown ni Tupac Shakur wa kizazi hichi cha muziki sababu anajua kuperforme, anaandika, anaimba,anarap na kuigiza.