Jumatano , 18th Feb , 2015

Msanii wa muziki Rashid Makwiro, maarufu zaidi kama Chidi Beenz leo hi amekiri mahakamani mashtaka matatu yanayomkabili.

Chidi Beenz (kulia)

Mashitaka hayo ni pamoja na kukutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine yenye thamani ya shilingi 30,638, bangi ya shilingi 1720 ma vifaa vya kutumia dawa hizo.

Chidi amekiri mashtaka hayo mbele ya hakimu Warialwande Lema baada ya kusomewa upya hati yake ya mashtaka, ambapo sasa atasubiri mahakama kusikiliza maelezo ya awali ya kesi hiyo Februari 23 mwaka huu.

Ombi la kusomewa mashtaka upya liliombwa na Wakili wa Serikali, Diana Lukondo ambapo hakimu aliridhia, na dhamana ya Chidi inaendelea ambapo atarejea tena mahakamani hapo Jumatatu ijayo.