Chidi Beenz
Chidi amekamatwa leo mchana akiwa katika sehemu ya kuondokea uwanjani hapo ambapo alifanyiwa upekuzi na kubainika amebeba dawa hizo ambapo ni kete 14 za dawa za kulevya kwenye mfuko wa shati lake na misokoto miwili ya bangi.
Kete hizo 14 za dawa za kulevya zilikuwa zimefungwafungwa na nailoni na pia amekutwa na vifaa vingine vinavyohusiana na watu wanaotumia dawa za kulevya, kuna kigae pia kijiko na Chid Benz amekiri mwenyewe kuwa hizo dawa ni zake pamoja na hivyo vifaa