Jumamosi , 23rd Mei , 2015

Msanii anayekuja juu kwa kasi katika miondoko ya Hip Hop, Chibau ameamua kutia nakshi muziku huo kwa kutengeneza kolabo na mwanamuziki wa dance.

Chibau na Jacky Chant

Chibau mtoto wa Pwani, amesema kuwa kufanya kazi na msanii wa dance Jacky Chant, binafsi akiwa kama msanii anaye fanya rap, ni hatua ambayo ameichukua kucheza na wigo mpana uliopo ndani ya muziki na kuleta ubunifu, ladha na utofauti zaidi katika kazi yake, kupitia project yake kubwa kabisa ya Nipokee.

Chibao amesema kuwa, Nipokee imekuwa ni kazi yake kubwa ambayo imefanikiwa kuisukuma mbele sanaa yake ndani ya wiki 2 tu, ikiwa ni project ambayo imesukwa baada ya kushauriana na mtayarishaji Mr T Touch kusuka mdundo ambao unaweza kumleta pamoja rapa pamoja na mwimbaji wa dance, kitu ambacho kimefanikiwa kwa kiasi kikubwa.