Jumamosi , 23rd Jan , 2016

Staa wa muziki Chege, ameweka wazi kuanza kufurahia matunda ya kuwekeza pesa nyingi kutengeneza rekodi yake kubwa ya Sweety Sweety, ambapo amesema kwa muda mfupi asivyotegemea, rekodi hiyo imefanikiwa kuingia katika top 10 ya Africa Music Chart.

Chege

Chege ameeleza kuwa, anakumbuka kutumia dola 1500, pesa ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 3 na laki 2 za kitanzania kwa gharama na utayarishaji wa rekodi hiyo (Audio) pembeni ya gharama za video, usafiri malazi na mahitaji ya muongoza video, uwekezaji ambao matokeo yake ni kama anavyoeleza mwenyewe hapa.