Jumanne , 18th Feb , 2025

Mastaa wa muziki Duniani Jay Z Mkewe Beyonce na familia yao wamepokea vitisho vya kuuawa sababu ya madai ya uovu,uongo na ubakaji baada ya jina la JayZ kutajwa kuhusu hilo.

Picha ya Jay Z na Beyonce

Jay Z anadai amepokea vitisho hivyo mitandaoni ambapo vimeanza baada ya kushutumiwa pamoja na Diddy kumshambulia na kumbaka mtoto wa miaka 13 kwenye tafrija ya Video Music Awards 'VMAs' mwaka 2000.

Wengi wanataka Jay Z atupwe gerezani mpaka kuzimu,wengine wanamuita shetani na jitu gaidi lakini amekana madai ya taarifa hizo akisema zina lengo kumchafua na kumdhalilisha.