Jumatano , 30th Apr , 2014

Staa wa muziki wa nchini Uganda, Jose Chameleone ameripotiwa kuwa katika mpango wa kurejea katika jumba lake lililopo huko Seguku nje kidogo ya jiji la Kampala nyumba ambayo alilazimika kuihama mwanzoni mwa mwaka 2013 kwa sababu za kuisalama.

Jose Chameleone

Chameleone ambaye amekuwa akihama katika makazi kadhaa tangu alipohama katika jumba hili, ametajwa kufikia maamuzi haya baada ya kuona kuwa sasa kila kitu kimerudi katika mstari, suala kubwa likiwa ni kuimarisha ulinzi wake pamoja na familia yake.

Chameleone alilazimika kuihama nyumba hii hasa baada ya mtu mmoja ambaye alifahamika kwa jina la Robert Karamagi kuvamia nyumba hii kwa lengo la kutaka kufanya uhalifu, na baadaye kupoteza maisha akiwa katika nyumba hii baada ya kuungua moto.