Jumamosi , 29th Mar , 2014

Muda mchache kabla ya kuanza kwa onyesho kubwa la Tubonge la msanii Jose Chameleone huko Uganda,

Afisa akiweka gari la Chameleone kizuizini

Muda mchache kabla ya kuanza kwa onyesho kubwa la Tubonge la msanii Jose Chameleone huko Uganda, msanii huyu alijikuta akipata chngamoto kutoka kwa mamlaka ya mapato ya nchini Uganda URA, ambao wameweka gari yake aina ya escallade kizuizini kwa madai ya kiasi kikubwa cha kodi ambacho wanamdai msanii huyu.

Tukio hili liliingilia ratiba ya mazoezi ya msanii huyu muda mchache kabla ya onyesho lake lililofanyika kwa mafanikio makubwa, ambapo baada ya mabishano ya hapa na pale, msanii huyu alikubali kuwaachia gari hilo mpaka pale watakapofikia suluhu ya jambo hili.

Chameleone mwenyewe amesema kuwa, hana tatizo lolote katika swala zima la kulipa kodi huku akiidai mamlaka hiyo kutolea vigezo walivyotumia kupata jumla ya shilingi milioni 7 za Uganda ambazo ndizo pesa wanazomdai.