Jumatatu , 18th Mei , 2015

Staa wa muziki wa nchini Uganda, Jose Chameleone amewataka mashabiki wake na wale wa aliyekuwa mdogo wake, marehemu AK47 kutoa ushirikiano katika kumsaka kijana anayefahamika kwa jina Mumbeere.

kijana anayesakwa kwa mauaji ya msanii AK47 wa Uganda, Mumbeere

Kwa mujibu wa taarifa za awali, Mumbeere ndiye anayehisiwa kusababisha kifo cha kusikitisha cha AK47 miezi miwili iliyopita, alikuwa mfanya usafi katika ukumbi wa starehe wa Dejavu ambapo ndipo AK47 alipopoteza maisha na mpaka sasa kijana huyo anahisiwa kukimbilia katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kwa mujibu wa kile alichosema Chameleone, zawadi nono itatolewa kwa yeyote atakayewezesha kupatikana kwa Mumbeere,
hatua ambayo itakuwa ni muhimu katika kuhakikisha haki inapatikana na mkanganyiko kuhusu kifo chake pia unafumbuliwa.