Jumanne , 12th Jan , 2016

Mwimbaji maarufu wa muziki wa injili nchini mhandis Carlos Mkundi ameamua kuupa kipaumbele kuendeleza muziki huo kwa kuweza kusaidia waimbaji mbalimbali kwa kuanzisha kampuni itakayokuwa ikitoa sapoti kwa wasanii na vikundi mbalimbali vya kwaya.

Mwimbaji maarufu wa muziki wa injili nchini Inginia Carlos Mkundi

Carlos ambaye hivi sasa anafanya vyema na video za nyimbo zake Moyo Wangu wa kuabudu na Nimetoka Mbali ambazo zimemtangaza katika sekta ya gospel, ameiambia enewz kuwa project hii kubwa itahusisha pia kuanzisha jarida litakalokuwa mahususi kwa ajili ya kuutangaza muziki huo na mchango wao katika jamii wanayoishi nchini.