Jumatatu , 24th Nov , 2014

Msanii wa muziki Bwana Misosi, anatarajia kutoka na ngoma inayokwenda kwa jina 'Nikifa Sitaki' Promo ikiwa ni ujumbe muafaka kugusia mtazamo tofauti juu ya matumizi ya kazi za wasanii hasa pale inapotokea kwa bahati mbaya wamefariki.

msanii wa bongofleva nchini Bwana Misosi

Kazi hii yenye ujumbe wa aina yake imefanywa na Misosi kwa kushirikiana na Banza Stone na msanii mkali wa bendi anayefahamika kwa jina Atanas na kuhusiana na Ujumbe na kilichomsukuma kufanya kazi kama hii, Misosi anaeleza zaidi.