Jumatatu , 18th Jan , 2016

Fredrick Bundala a.k.a Sky Walker ni mwandishi wa habari na blogger anayeishi jijini Dar es Salaam ameamua kuonesha uwezo wa kuyazungumzia Maisha, Mapenzi na Maumivu kupitia vitabu vyake ambapo vitabu hivyo vinavyoyaangaza maisha ya mastaa wakubwa

Kitabu cha kwanza cha Maisha, Mapenzi na Maumivu ameamua kuyaangalia maisha ya wanandoa kwenye muziki wenye nguvu zaidi duniani, Sean Carter maarufu kama Jay Z na Beyonce Knowles.

Katika kitabu hiki amezungumzia undani wa maisha yao, ukubwa wao katika muziki na biashara na uhusiano wao pamoja na maumivu na majaribu waliyoyapitia katika ndoa yao kiasi cha kuwa katika hatari ya kuvunjika.

Fredrick Bundala anaelezea kitabu hiki kwa sasa unaweza kukipata katika maduka mbalimbali au waweza wasiliana naye zaidi kama maelekezo yalivyo kwenye picha