Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Brenda Fassie

Ijumaa , 16th Feb , 2018

Miaka ya 2000 kurudi chini hakuna harusi utakayohudhuria bila kusikia nyimbo zake zikipigwa, au hakuna nyumba yenye redio au television iliyokosa albam yake hata moja, na watoto wengi walisikika wakiimba 'vulindela' bila hata kujua nani kaimba, na an

Anaitwa Brenda Nokuzola Fassie , alizaliwa Novemba 3, 1964 huko Langa Cape Town nchini Afrika Kusini, akiwa mtoto wa mwisho wa familia yenye watoto 8, jina la Brenda alilopewa lilitokana na wazazi wake kuwa mashabiki wa mwanamuziki wa Marekani Brenda Lee.

Baba yake alifariki akiwa na miaka miwili na kulelewa na mama yao pekee, ambaye alikuwa mcheza piano. Brenda alikuwa na kipaji tangu utotoni na kuanza kuimba na mama yake kwenye sehemu mbali mbali ambazo watalii walikuwa wanaenda.

Akiwa na miaka 16, Brenda Fassie tayari alikuwa na uwezo mkubwa wa kuimba na hata kuwa na bendi yake ya kitaa iliyoitwa 'The Tiny Tots'. Umaarufu wa Brenda ulianza kusambaa sehemu mbali mbali za Afrika Kusini na kumfikia producer wa muziki Koloi Lebona kutoka Johanesburg, na kuamua kwenda kwenye familia ya Fassie na kukutana na Brenda, na hatimaye kukubaliana kuondoka naye kwa ajili ya kuendelea na masomo na kufanya muziki Soweto.

Brenda akapata fursa nzuri ya kufanya kazi zake za muziki na kuwa maarufu zaidi. Alipomaliza mkataba na Lebona alianzisha bendi yake nyingine 'Brenda and the Big Dudes, na kurekodi hit song 'Weekend special' mnamo mwaka 1983, na kuwa rekodi iliyoongoza kwa mauzo Afrika Kusini, na kumpa ziara za kimuziki sehemu mbali mbali duniani.

Pamoja na bendi lakini Brenda alijiimarisha vizuri kama solo artist kwenye muziki wa Pop aliochanganya na mahadhi ya Afrika Kusini huku nyimbo zingine akiimba kwa lugha mbali mbali ikiwemo kingereza, Kiswahili, Kizulu na Xhosa.

Brenda alizidi kuachia kazi nzuri zilizofanya vizuri kwenye mauzo, nyimbo ambazo zilibeba jumbe mbali mbali kama za kupinga ubaguzi wa rangi, umoja, mapenzi na masuala ya kifamilia.

Maisha yake binafsi yakawa kwenye vyombo vya habari kama wasanii na watu wengine maarufu, mwaka 1989 aliolewa na Nhlanhla Mlambo na ndipo majanga yakaanza kumuandama, kwani mwaka uliofuata baada ya kuoana alishtakiwa kwa utapeli, na Agosti 1990 wawili hao waliachana.

Brenda alianza kutumia madawa ya kulevya pamoja na pombe kali na kuwa mlevi kupindukia, kitendo ambacho kilianza kumshusha kwenye kazi zake, huku wengine wakisema ndio mwisho wa 'Queen of Pop'. Skendo hazikuisha kumuandama kwani baada ya kuachana na mume wake alikumbwa na skendo chafu ya ngono ya kujihusisha kwenye mapenzi ya jinsia moja, na vyombo vya habari kuliweka kwenye 'front page'.

Matumizi ya madwa ya kulevya yalimuweka pabaya zaidi na mwaka 1995 kuamua kwenda 'sober house'. mwakaa uliofanya alifata 'comeback' ya nguvu huku akifanya kazi na mwanamuziki wa Congo ambaye ameshafariki Papa Wemba, na kuwa-prove wrong wale waliosema ameshaishiwa kwenye muziki, baada ya albam alizoachia kama 'Memeza' aliyoifanya na producer maarufu Afrika Kusini, Chicco, kufanya vizuri sokoni na kumpa tuzo kama Kora, SAMA na tuzo zingine za ndani.

Kitu ambacho wengi walikuwa hawajui baada ya kurudi kwenye game ni kwamba alikuwa akiendelea kutumia madawa ya kulevya, na mwezi April 2004 alikimbizwa hospitali baada ya kupata heart atack, iliyomplekea kuwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi, na baada ya wiki alifariki dunia mnamo May 9, 2004.

Baada ya kifo chake madaktari waligundua madawa ya kulevya aliyokuwa akitumia ndio yalimletea tatizo la moyo, na zaidi aliyotumia usiku wa siku aliyokimbizwa hospitali, alitumia cocaine ambayo iichanganywa na sumu ya panya.

Nchi ya Afrika Kusini ilimpenda sana Brenda Fassie akiwemo aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Nelson Mandela, na alipofariki serikali ilitengeneza sanamu maalum iliyowekwa kwenye jumba la maonyesho kumuenzi mwanamuziki huyo wa Pop aliyetikisa Afrika na dunia, aliyepewa jina la 'Madonna of the township'.

Brenda alipofariki aliacha mtoto wa kiume aliyekuwa na miaka 19 anayeitwa Bongeni Fassie.

HABARI ZAIDI

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu