"Bora nifanye kazi Konde Gang kuliko Benki" - AT

Ijumaa , 23rd Jul , 2021

Mfalme wa muziki wa mduara Ally Tolu AT amesema ni bora afanye kazi kwenye lebo ya Kondegang Worldwide kuliko kufanya kazi Benki kwa sababu Kondegang wanamuheshimu na wanamsapoti kwenye kazi zake.

Msanii AT kulia kushoto ni Harmonize

AT anasema hajasainiwa Kondegang ila ni mwanafamilia wa lebo hiyo muziki na kazi zake zitakuwa zinahusisha Kondegang kwa asilimia 95.

"Mimi sijasainiwa Konde Gang lakini ni mwanafamilia kazi zangu nafanya nawahusisha wao kwa asilimia 95, acha niwaambie ukweli kwa mimi ni bora kufanya kazi na Konde gang kuliko kufanya kazi Benki" amesema AT 

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.