Ijumaa , 26th Jun , 2015

Baada ya mapokezi mazuri kabisa ya rekodi ambazo ameziimba kwa lugha ya Kiswahili, star wa muziki wa nchini Uganda, Bobi Wine ameonesha muelekeo wa kuishikilia lugha hiyo katika sanaa yake, hatua ambayo imeendelea kumuweka karibu na mashabiki wengi

Bobi Wine

Tathmini hii ni kutokana na kuendelea kushika chati kwa rekodi yake ya Nakumiss, ikiwa ni ya pili kuifanya kwa lugha hii adhimu, baada ya ile ya Paradiso ambayo alieleza kuwa aliifanya kwa msukumo wa mapenzi ya marehemu baba yake.

Hata hivyo, staa huyo ambaye kwa sehemu kubwa hutumia lugha ya Luganda katika rekodi zake, amekuwa akishikilia lugha yake ya asili katika ngoma zake kwa lengo la kujitofautisha na wasanii wenzake kutoka nchi hiyo ambao huchanganya lugha katika muziki wao.