Jumamosi , 12th Oct , 2024

Binti wa staa wa RnB R Kelly, Buku Abi anasema yeye pia ni muathirika wa unyanyasaji wa kingono na jinsia aliofanyiwa na baba yake huyo wakati akiwa na umri mdogo.

Picha ya R Kelly na binti yake Buku Abi

Mtoto wake huyo amefichua madudu hayo kupitia Documentary ya “Karma A Daughter’s Journey” ambayo inaeleza amefanyiwa vitendo hivyo akiwa na miaka 10 tu.

"Kwa muda mrefu, sikutaka kuamini kwamba alinifanyia, sikujua kwamba hata kama angekuwa mtu mbaya na kunifanyia jambo fulani kwangu".

"Niliogopa sana kumwambia mtu yeyote hata mama yangu niliogopa kumwambia"-amesema Binti wa R Kelly

Kwa sasa R Kelly anatumikia hukumu yake ya kifungo kwa mashtaka ya ulaghai na biashara ya ngono inayohusisha unyanyasaji wa kingono kwa watoto.