Kwa mujibu wa taarifa Beyoncé amevunja mkataba na meneja wake wa miaka mitano, Lee Anne Callahan-Longo, na kwa sasa anafanya kazi na Steve Pamon aliyekuwa mkuu wa masoko kwa upande wa michezo na burudani wa benki maarufu nchini Marekani.
Beyoncé alimchukua Pamon kusimamia kampuni yake ya Parkwood Entertainment inayofanya kazi ya usimamizi, utengenezaji muziki, ziara, picha na kazi nyingine, ikikumbukwa kuwa jamaa huyo ndiye aliyesaidia kupatikana kwa udhamini wa ziara yao kubwa ya On The Run.





