Alhamisi , 26th Mar , 2015

Staa wa muziki Moses Ssali maarufu zaidi kama Bebe Cool kutoka nchini Uganda, amechaguliwa kuwania tuzo kubwa za muziki ya nchini Australia.

msanii wa nchini Uganda Bebe Cool

Jina la Bebe Cool linaingia katika kinyanganyiro hicho sambamba na majina ya wasanii wengine zaidi ya 30 kutoka sehemu mbalimbali duniani wakiwepo P-Square, Fuse Odg na Timaya kati ya wengine.

Wasanii hawa watawezeshwa kushinda tuzo hizo kupitia kura za mashabiki zao ambazo utaratibu wa kuzipiga utawekwa wazi hivi karibuni.