Jumanne , 27th Sep , 2016

Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) kupitia mkuu wake wa matukio Kurwijira N. Maregesi , wametoa msisitizo kwa wasanii kujisaji kwenye baraza hilo, ili waweze kushiriki EATV AWARDS.

Mkuu wa matukio BASATA Kurwijira N. Maregesi

Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Bw. Maregesi amesema ni muhimu kwa wao kufanya hivyo, kwani kuna umuhimu mkubwa kwa wasanii kushiriki EATV AWARDS.

“Sharti ni lile lile kwamba hakuna atakayeruhusiwa kushiriki hizi tuzo kama hajasajiliwa, wasajiliwe Baraza la Sanaa la Taifa, lipo kwa ajili ya wasanii wote, tuzo hizi ni muhimu sana, zinakupa platform ya kuonekana sehemu nyingine, hao wengine wameweza kuonekana huko wanakoenda kwa sababu ya tuzo zetu nyingine, na sasa zipo hizi nyingine zimeanza, hizi za East Africa Tv, ni muhimu sana washiriki kwani ni haki bin haki”, alisema Maregesi.

Tags: