Alhamisi , 22nd Oct , 2015

Staa wa muziki Barnaba Classic, ameweka wazi kikosi cha wasanii ambao kwa sasa tayari wamekwisha mwaga wino kufanya kazi chini ya studio anayomiliki ya Hightable Sound ambayo imekwishaanza kuonesha matunda yake katika tasnia ya muziki Tanzania.

Staa wa muziki nchini Barnaba Classic

Barnaba ameweka wazi kuwa wasanii hao wanaofanya kazi chini yake kwa sasa ni pamoja na rapa Ice Boy, Asia, na vilevile msanii kutoka Njombe ambaye anasimama kwa jina la Mula Flavour, na hii ni kama anavyoeleza mwenyewe hapa.