Jumatano , 12th Mar , 2014

Msanii Bobi Wine pamoja na mkewe Barbie wameendelea kuwa na mchango wenye manufaa kwa jamii, na hii ni kutokana na hatua yao ya hivi karibuni ya kuanza kujihusisha na mpango wa kusaidia vijana nchini Uganda.

Katika mpango huu uliopatiwa jina “Save the Children” Everyone is Me, Barbie ametangazwa kama balozi rasmi ambaye kazi yake itakuwa ni kuwahamasisha wanawake wote huko nchini Uganda, kutafuta huduma za uhakika na salama za uzazi ili kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga hususan katika kipindi cha kujifungua.

Kupitia mpango huu, Barbie pamoja na Bobi Wine hivi karibuni walipata kutembelea hospitali mbalimbali ikiwepo ile ya Nakaseke ili kujionea hali halisi ya tatizo ambalo wanapambana nalo.