
Khloe amesema hayo alipokuwa akifanya mahojiano juu ya hatma yake na mume wake huyo ambaye kwa sasa anaendelea na matibabu baada ya kunusurika kifo kutokana na kuzidisha matumizi ya dawa.
“Bado nimeolewa kwa sababu nyingi, hata kama Lamar atakuwa sawa kwa asilimia 100, ana mambo mengine mengi ya kushughulikia kabla hajachukua mahusiano yoyote, natumai watu wanaelewa hilo haliko kwenye mawazo yetu, kuna vitu vingi vya muhimu, vingi vya matibabu”, alisema Khloe alipokuwa akisaini kitabu chake ambacho amekitoa siku chache zilizopita.
Khloe alikuwa kwenye mchakato wa talaka na mume wake huyo kabla hajakutwa na matatizo ya kiafya, hivyo kuamua kufuta mchakato huo huku akiendeleza mahusiano na mpenzi wake mpya James Harden, ambaye kwa mujibu wa Khloe amesema amekuwa msaada mkubwa na muelewa kwa kipindi chote ambacho Khloe anamuuguza mume wake Lamar Odom.