
Bad Black chini ya ulinzi
Kesi hii inakuja baada ya mahakama kuzuia uhalali wa gari hii kutumika kama bondi kutokana na mali zote za mwanadada Bad Black kuwa kizuizini kutokana na kesi ya awali ya ubadhirifu wa shilingi bilion 11 inayomkabili, kesi ambayo alifunguliwa na aliyekuwa mpenzi wake, David Greenhalgh.
Kwa sasa bado Bad Black anatumikia kifungo cha miaka minne gerezani, huku akiwa na mlolongo wa mashtaka mengine ambayo yanazima ndoto zake za kurejea maisha yake ya kifahari aliyokua anaishi miaka ya nyuma.