Jumanne , 10th Oct , 2023

Baba mzazi wa staa wa muziki duniani Drake mzee Dennis Graham amewajibu mashabiki na wadau wa muziki wanaomchukia mtoto wake kwamba kama hawapendi anachofanya waachane naye.

Picha ya Drake na baba yake mzazi Dennis Graham

Baba huyo mzazi wa Drake ameshusha ujumbe huu kwa wote wanaomchukia mwanaye akiandika 

"Ni aibu kwamba msanii mchanga hawezi kufanya mambo yake mwenyewe na kufurahia bila chuki za watu wa zamani kwa sababu wao hakuna walichofanya".

"Naumwa kwa sababu ya hawa watu wa zamani wanaomchukia mwanangu, kama haupendi anachofanya endelea na mambo yako, hakusumbui wala nini".

Baba wa Draka ameelezea hilo baada ya rapa wa zamani ambaye ni mtangazaji kwa sasa Marekani Joe Budden kuikosoa Album mpya ya Drake 'For The All Dogs' akisema anaimbia watoto hivyo aandike mistari ya watu wazima kwa sababu umri wake umeenda.