Picha ya msanii Lil Baby
Katika video hiyo mmiliki alionyesha viatu vingi, nguo na vitu vingine akidai vilisalia baada ya rapa huyo na timu yake kuondoka katika nyumba hiyo inayokodishwa kwa takriban dola 10,000 sawa na Tsh Milioni 26.
Baadhi ya watu waliona kitendo hicho kama cha kawaida kinachoonyesha maisha ya mastaa, huku wengine wakikosoa uamuzi wa mmiliki huyo kuweka hadharani mali za mteja wake, wakisisitiza umuhimu wa kuheshimu faragha.
Baadae Lil Baby alithibitisha kuwa yeye na timu yake kweli waliacha baadhi ya vitu katika eneo hilo, jambo lililoongeza zaidi mjadala kuhusu tukio hilo mtandaoni.





