Baby J akiwa katika pozi visiwani Zanzibar
Baby J ambaye muda mwingi yupo maskani yake Zanzibar amesema sababu ya kukaa zaidi ya mwaka bila kuachia ngoma mpaka watu wanadhani ameacha muziki ni matatizo binafsi ambayo yamekwishakaa sawa na sasa anarudi mzigoni.
Lakini Baby J hakutaka kuweka wazi jina la Project anayokuja nayo na kusema sasa yupo chini ya usimamizi ambao unamuongoza kwa hiyo soon mambo yatakua hadharani so funs wake wawe tayari kumpokea.