Jumatano , 26th Nov , 2014

Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Avril amekanusha kuwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na rapa G-Kon wa nchini humo, ambaye mara kwa mara amekuwa akidai kuwa Avril amemtenda na kusaliti penzi lake.

msanii wa muziki wa nchini Kenya Avril

Avril amedai kuwa, mapenzi na mahusiano yanayomhusu yeye ambayo G-Kon amekuwa akiyazungumzia ni kitu ambacho kipo ndani ya kichwa chake mwenyewe na hakijawahi kuwa katika uhalisia.

Avril pia amesisitiza kuwa hawezi kuwa na heshima na wala hawapendi watu wanaoishi maisha ya 'sinema' ya kutengeneza, huku akidhihirisha kukerwa sana na kile anachokifanya G-Kon.