Alhamisi , 25th Jan , 2018

Msanii wa muziki wa bongo fleva Aslay, amemtaja mtu ambaye alikuwa akimfikria wakati anaimba wimbo mpya wenye ujumbe mtamu wa mapenzi 'Subalkheri' alioshirikiana na Nandy.

Akizungumza kwenye kipindi cha 5SELEKT kinachorushwa na East Africa Television, Aslay amesema mtu pekee ambaye alikuwa kaimfikiria wakati akiimba wimbo huo ni mama yake mzazi, ambaye ameshafariki dunia.

“Nilikuwa namfikiria mama, kwa sababu enzi hizo alikuwa hai alikuwa anasikiliza, nikawa natamani kama angeisikia mwanae nikiimba hii nyimbo”, amesema Aslay.

Aslay sio mara ya kwanza kumtaja mama yake kwenye suala kama hilo, kwani ndiye mtu pekee ambaye alikuwa naye karibu na kumueleza mambo yake ya ndani, lakini kwa sasa hayupo tena duniani.