Ijumaa , 30th Mei , 2014

Muigizaji wa kike wa Kenya anayefanya shughuli zake za ugizaji nchini Ujerumani Ashley Toto ametua ndani ya Afrika Mashariki akiwa na lengo la kuweza kukuza soko zaidi la filamu na huku akitaraji kuja kufanya kazi na wasanii kutoka Tanzania.

Ashley amefunguka na kusema kuwa lengo lake la kufanya kazi na watanaznia kutokana na sasa soko la filamu la Tanzania limepanuka zaidi lakini pia kuweza kutafuta uwanja mpana zaidi wa kukuza kazi zake ambazo anaamini kwa kufanya kazi na watanzania zitakubalika zaidi.

Aidha, Ashley alikataa habari zilizosambaa kwamba yupo katika mahusianao ya kimapenzi na msanii Bob Junior kwani Bob ni rafiki yake tu.
zaidi sikiliza hapa.