Jumamosi , 26th Apr , 2014

Msanii wa muziki Amileena kutoka nchini Kenya, amejipanga tayari kwaajili ya kuachia video yake mpya ya ngoma inayokwenda kwa jina Naona Bado kwa namna ya kipekee, ambapo tukio hili litafanyika katika harusi ya bosi wa lebo ya Grandpa, Refigah.

Amileena

Katika harusi hii, mbali na uzinduzi wa video hii mpya ya Amileena, Refigah mwenyewe ameongezea kuwa, sherehe hii itapambwa na showz kutoka kwa wasanii mbalimbali wanaofanya vizuri muziki huko nchini Kenya.

Uzinduzi wa video hii unatarajiwa kuwa ni wa aina yake, na unatarajiwa kufanyika mbele ya wageni zaidi ya 2000 ambao wanatarajiwa kuhudhuria harusi ya Refigah.

Tags: