Jumatatu , 2nd Sep , 2024

Aika Nahreel tumeagizwa upendo, hiyo ni Intro waliyoanza nayo Navy Kenzo (Aika Nahreel) na wamemaanisha ukweli sababu upendo umetawala katika mahusiano yao kwa muda wa miaka 16 sasa.

Picha ya Aika na Nahreel

Miaka 16 ya upendo wao bila kusikia kuachana kwao, ugomvi, kiki au maisha yao binafsi. Wameacha watu wajifunze upendo au mahusiano na kuenjoy muziki mzuri kupitia wao.

Story ya Aika na Producer Nahreel ilianzia Manzese nyumbani kwa Madee na Nay Wa Mitego mpaka chuoni India, kisha kurejea Tanzania kufanya muziki.

Wanatajwa kuwa ni Couple bora ya muda wote Tanzania, pia ndiyo mastaa wanaoweza kushauri watu au mastaa wenzao jinsi ya kuishi na mpenzi kwenye mahusiano.

Katika miaka yao 16 ya kuwa pamoja wamebarikiwa watoto wawili na Hits kibao kama Katika, kamata chini, game, moyoni, fella, manzese, company, lini, morning, bajaji na zingine kibao.