Ijumaa , 24th Jun , 2016

Mwanamuziki wa kizazi kipya nchini Afande Sele ameongea na Enews na kuongelea swala la wasanii wengi wa kitanzania 'kufeki' maisha yao halisi ikiwemo kubadili hata rangi za ngozi zao na kujiongezea weupe na wakati mwingine hata kubadilisha asili yao.

AFANDE SELE

Hata hivyo Afande Sele amesema ni kutokana na uelewa wao kuwa mdogo kwa kuwa kubadilisha muonekano hakuchangii kazi anayofanya msanii kuwa bora, bali ubora wa kazi yenyewe ya sanaa ni kutokana na ubunifu na utofauti katika kazi.

Afande sele amewataja baadhi tu ya wasanii wa kiafrika ambao wamefanya vizuri kimataifa kama kina MIRIAM MAKEBA, MADONA na wengine wengi bila kujibadilisha wala kuongeza kitu chochote katika ngozi zao au mionekano yao.

Afande amemaliza kwa kuwasihi wasanii wenzake kupunguza kufeki maisha yao.