Ijumaa , 15th Dec , 2017

Msanii Abdukiba kutoka ‘Label’ ya ‘Kings Music’ amekanusha maneno ya watu kuwa bosi wa ‘Label’ hiyo Alikiba ambaye pia ni kaka yake alikuwa akimzuia kwenye muziki. 

Abdukiba amefunguka hayo leo wakati akifanya mahojiano na eNEWZ ya East Africa Television ambapo amesema kuwa Alikiba alikuwa akimtengenezea njia nzuri ya kuja kufanya mziki mzuri na ni mtu ambaye anatakiwa kusikilizwa kwenye game.

Mkali huyo ameongeza kuwa Alikiba alimuambia apumzike kidogo asiachia nyimbo ili akirudi aachie nyimbo nzuri na mashabiki wake watampokea kwa mikono miwili lakini pia watakuwa wamemmisi katika game, hivyo hata kama kutakuwa na changamoto yeyote katika mziki wake itakuwa rahisi kupata maoni.

Abdukiba ambaye anatamba na ngoma yake mpya ‘Single’ aliyomshirikisha Alikiba amesema pamoja na kukaa kimya kwa mda mrefu kwa ushauri wa Alikiba lakini pia kuna mambo yanayohusiana na sanaa yake ambayo alikuwa anayaweka sawa ili mradi kujipanga kwani mziki wa sasa hivi umebadilika na una ushindani mkubwa.