Jumanne , 11th Mar , 2014

Msanii wa miondoko ya Hip Hop kutoka Kenya, Abbas Kubaff anatarajia kuonyesha sehemu nyingine ya usanii wake, ambapo mwezi ujao atafanya maonyesho makubwa ya kazi za sanaa ya uchoraji kwa kutumia rangi ambazo amezifanya.

Msanii huyu ameweka wazi kuwa, amekuwa akitumia muda mwingi kutengeneza kazi hizi za uchoraji ambazo ni kipaji chake kingine, na sasa ana kazi za kutosha ambazo ataziweka hadharani kupitia maonyesho haya.

Msanii huyu pia ameweka wazi mpango wa kuzindua albam yake mpya ya muziki baada ya maonyesho haya katika kuthibitisha ukongwe na uwezo wake mkubwa wa kuifanya sanaa.