
Filamu hii mpya ambayo itamuuzisha sura vilivyo 2Face, imepatiwa jina Make a Move ikiwa inabeba maudhui ya kimuziki, ikiwa na lengo kubwa la kufundisha watazamaji wake juu ya mambo muhimu katika kucheza muziki.
Filamu hii inatarajiwa kutoka tarehe 6 mwezi Juni, na ndani yake imeshirikisha pia mastaa wengine wa filamu kutoka Nigeria, akiwepo Majid Michel, Beverly Naya, Wale Adebayo na Tina Mba.