Ijumaa , 18th Jul , 2014

Msanii wa muziki nyota nchini Uganda Jose Chameleone amejiwa juu na mashabiki wake ambao wamemlalamikia kuhusu tamasha lake la muziki ambalo amepanga kutoza kiasi cha shilingi milioni moja za Uganda.

msanii Jose Chameleone wa Uganda

Chameleone ameweka wazi kuwa tamasha lake alilolibatiza jina '1 Man, 1 Show, 1 Thousand' ni tamasha lenye gharama kubwa kuwahi kufanyika likiwa ni mahususi kwa ajili ya harambee ya kuchangia kuukuza muziki wa nchini Uganda.

Chameleone ameelezea kuwa tayari kuna orodha kubwa ya wasanii watakaopaform wakiwemo Papa Cidy, Radio & Weasel na wengineo wengi.