Jumatatu , 17th Dec , 2018

Mlimbwende maarufu kwenye video za bongo fleva, Tunda 'The Boss Babe', ameweka wazi kiwango chake cha ufaulu alipohitimu kidato cha nne, ambacho kimezua gumzo kutokana na upekee wake.

Akizungumza na Big Chawa wa Planet Bongo ya East Africa Radio, Tunda amesema kuwa yeye hakufeli kidato cha nne, bali alifaulu kwa wastani wa division two ya mia tano (500), na maongezi yao yalikuwa kama hivi:

Big Chawa: Unaweza ukawaambia watu ulipata zero ya kwanza au four ya mwisho?
Tunda: Aaah wee, babu wee, sijapata zero.
Big Chawa: Ulipata four ya mwisho!?
Tunda: Nilipata division two,
Big Chawa: Two!?, Two ya ngapi!?
Tunda: Two ya mia tano

Msikie hapa chini