
Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akihutubia katika Maadhimisho ya wiki ya Ubunifu na Utafiti yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jijini Dar es Salaam.
Majaliwa ametoa agizo hilo wakati akihutubia katika Maadhimisho ya wiki ya Ubunifu na Utafiti yaliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa ni mgeni rasmi alisema kuwa amevutiwa na kauli mbiu ya maadhimisho hayo inayosema ‘utafiti na ubunifu kwa maendeleo ya viwanda na jamii Tanzania” kwani inaenda sambamba na mipango ya maendeleo ya taifa na ulimwengu.
“Niwaahidi kwa upande wa serikali tutaendelea kutenga bajeti yakutosha kama ambavyo ameeleza waziri Prof. Ndalichako, Serikali tunaona kuna umuhimu wa kuongeza bajeti, na waziri wa elimu upo hapa bunge la bajeti linaendelea hata kama wizara yako imepita basi rudi tena fanya mapitio na una nafasi nzuri li uweze kuongeza fedha kwenye dirisha hilo la utafiti, vyuo vikuu vyetu vinufaike na wale wote wanaojishughulisha na utafiti wanufaike kupitia serikali” amesemaMhe. Majaliwa
Pia Majaliwa amesema kuwa maonesho hayo ya tafiti yanatoa tumaini kwani zipo tafiti ambazo matokeo yake yataboresha maisha ya watanzania, huku akitoa rai kwa watafiti kuendelea kufanya tafiti mbalimbali na kutofungia matokeo ya tafiti hizo badala yake kuyaweka bayana kwa kuujulisha umma wa watanzania juu ya faida ya tafiti hizo.
“Nidhahiri Kupitia maonesho haya mmetupa matumaini makubwa na kutudhihirishia kuwa zipo tafiti nyingi ambazo matokeo yake yakiwekwa bayana nakutumika ipasavyo yataboresha maisha ya watanzania, Wakati tukifanya hayo yote, ni muhimu pia kujitayarisha kutumia kikamilifu matokeo ya tafiti zetu kama fursa au bidhaa adimu ya biashara” amesema Waziri Mkuu