Msigwa ateuliwa kuwa Msemaji wa serikali

Jumatatu , 5th Apr , 2021

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua  Gerson Msigwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa serikali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, Kushoto ni Msemaji wa Mkuu Serikali, Gerson Msigwa.

Kabla ya uteuzi huo, nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Dk Hassan Abbas ambaye ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

Awali Rais Samia amewateua makatibu wa kuu na manaibu Katibu wakuu wakiwemo  Dkt. Moses Mpogole, Prof.Riziki Shemdoe, Dkt.Laurian Ndumbaro, Tixon Nzunda, Prof.Godius Kahyarara, Emmanuel Tutuba, Sifuni Mchome, Dkt Abel Nkono Mkubi, Grace Maghembe na Adolf Ndunguru

Pia Rais Samia amemteua Dkt. Aifello Sichwale kuwa Mganga mkuu wa serikali na Dkt. Jabir Bakari Kuwe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Hata hivyo Viongozi walioteuliwa hapo jana tarehe 4/04/2021 wanatarajia kuapishwa kesho tarehe 6/04/2021  Ikulu,Dar es salaam.