Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Lissu aipa Serikali mtihani

Jumanne , 12th Sep , 2017

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara na Wakili wa kujitegemea Tanzania. Prof Abadallah Safari amesema wao kama CHADEMA hawana imani na uchunguzi utakaofanywa na jeshi la polisi au serikali kuhusu shambulio la kujaribu kumuua Mbunge Tundu Lissu.

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Prof Abadallah Safari

Akizungumza na wanahabari wakati wakitoa taarifa ya kamati kuu kupitia kikao walichokaa mwishoni mwa wiki iliyopita, Prof. Safari amesema kuwa wao hawana nia mbaya ya kutaka uchunguzi kufanywa na wachunguzi wa mambo ya nje lakini hii ni kutokana jinsi tukio lilivyotokea.

"Hatuna nia mbaya lakini sisi kama CHADEMA hatuna imani na serikali pamoja na jeshi lake la polisi katika uchunguzi wa jaribio la mauaji ya Mbunge wetu. Serikali pia  isipokubali kuleta wachunguzi kutoka nje tafsiri ni kwamba wanaogopa kuunguzwa na lipo jambo wanaloficha kuhusiana na shambulio la jaribio la kutaka kumuua ndugu yetu Tundu Lissu ambaye kwa sasa bado anapigana na kutaka kuokoa maisha yake kwani hali yake bado si nzuri" alisema Prof Safari.

Pamoja na hayo Prof. Safari amedai anamshangaa sana Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini , IGP Simon Sirro, kwa kauli yake ya kwamba Tundu Lissu hakufika kuripoti tukio la kufuatiliwa na watu asiowajua na kusema kuwa huko ni kutojua sheria ya mmwenendo wa makosa ya jinai.

Amesema kuwa Sheria hiyo inaeleeza namna jeshi lapolisi linavyotakiwa kufanya kazi zake na kwamba kutokana na aslimia 90 ya wananchi basi jeshi la polisi kazi yake ni kufuatilia  na kufanya upelelezi juu ya taarifa kwani wao ni walinzi wa amani na kuongeza kwamba Lissu tayari alieleza kila kitu lakini polisi hawakujali.

"Hatuamini kama walikuwa hawajui kama kuna taarifa Lissu alizitoa kuhusu yeye kufuatiliwa au waliamua tuu kutotilia maanani"  alisisitiza Prof. Safari.

Mbali na hayo Katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt. Vicent Mashinji ameeleza kwamba kwa sasa wanachohakikisha ni kwamba hospitali aliyopo Lissu inazidi kuimarishwa ulinzi lakini pia hatoweza kuzungumzia hali yake kwa undani kutokana pia na kuwepo watu wasiokuwa na nia njema.

HABARI ZAIDI

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi