
Wa pili kushoto Balozi wa Canada nchini Tanzania Pamela O'Donnell,na wa pili Kulia Balozi wa Uingereza nchini, David Concar wakiwa na Mkuu wa vipindi vya Radio wa East Africa, Lydia Igarabuza (Wa kwanza kulia}.
Wakizungumza mara baada ya ziara wameeleza kufurahishwa na mabadiliko ya teknolojia katika vyombo hivyo, pamoja na ufanyaji kazi katika vyombo hivyo vya habari.
Balozi wa Canada Nchini Pamela O'Donnell (wa kwanza kulia) akiwa na mtangazaji wa Kipindi cha MamaMia cha East Africa Radio Maryam Kitosi
Ikiwa leo ni siku ya maadhimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, mabolozi hao walipata wasaha wakuzungumza na wafanyakazi wa vyombo vya IPP Media kuhusu uhuru wa vyomBbo vya habari, huku wakigusia lengo lao la kufanya kazi na nchi nyingine katika kusaidia kuboresha uhuru wa habari.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar akielezewa jambo na Mkuu wa vipindi vya East Africa Radio Lydia Igarabuza
Pia wakielezea mtazamo wa vyombo vya habari nchini wamevipongeza na kuelezea kuwa vimejikita katika kuhabarisha umma huku habari zake zikijikita kutoka mamlaka husika na zile zitokanazo na maoni ya wananchi.
Naye Mkuu wa vipindi vya Radio wa East Africa, Lydia Igarabuza akitoa hoja juu ya kipi kifanyike katika tasnia ya habari ameeleza kuwa ipo haja ya kuboresha utaalum kwa waandishi katika maeneo mbalimbali ambapo maboresho hayo yote yanaweza yakafanyika kupitia program za kuwaongezea uwezo waandishi.