Jumanne , 27th Sep , 2022

​​​​​​​Rais wa zamani wa Afrika kusini Bw Jacob Zuma, amesema kwamba huenda akarejea tena kwenye ulingo wa siasa za nchi hiyo baada ya kulazimika kujiuzulu  mwaka 2018.

Bw. Zuma alijiuzulu kwa tuhuma za rushwa ambazo anakana mpaka sasa.  Amesema kwamba siku ya jumatatu alifuatwa na baadhi ya wananchama wa chama tawala nchini humo cha ANC , wakimtaka awe mwenyekiti wa chama hicho , ikiwa ni kuelekea mkutano wake mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi    Disemba mwaka huu.

Amesema kwamba hawezi kukataa wito huo endapo watamuhitaji kuja kukitumikia chama hicho kwa mara nyingine katika ufanisi. 

Ameongeza kuwa  chama cha  ANC kinapitia changamoto za umoja .